Riwaya ya Nguu za Jadi imeandikwa na Profesa Clara Momanyi,
mwandishi na mtafiti mwenye tajriba pana katika fasihi ya Kiswahili.
Miongoni mwa kazi zake ni Tamathali Katika Vitendawili (2001), hadithi
fupi Ngome ya Nafsi iliyochapishwa katika antholojia ya Mayai Waziri wa
Maradhi na Hadithi Nyingine (2004), Tumaini (2005), Siku ya Wajinga
(2005), na Nakuruto (2009). Vilevile ameandika makala mengi ambayo
yamechapishwa katika majarida mbalimbali ya usomi. Kwa sasa yeye ni
mhadhiri katika chuo kikuu cha Kenyatta jijini Nairobi. Kupitia riwaya hii,
anaangazia matukio katika nchi ya Matuo ambayo inapitia kipindi kigumu
miaka mingi baada ya uhuru. Miongoni mwa matatizo hayo ni ufisadi,
ukabila, mila, na ufasiki. Matatizo haya yanasambaratisha asasi muhimu
za jamii ikiwemo familia na uongozi. Hata hivyo, mwandishi amefanikiwa
kuielekeza jamii kwa kuonyesha umuhimu wa mapinduzi katika kujenga
jamii mpya yenye matumaini. Kupitia wahusika kama Mwamba, Lonare,
Mashauri, na Mangwasha, mshikamano wa kijamii unajengwa na kubomoa
uovu uliosaki katika jamii. Yote haya yamefumwa kistadi kwa kutumia
ujuzi mkubwa wa fani zilizokolezwa mandhari, uhusika, na mbinu murua
za lugha na za sanaa. Waama, riwaya hii ni tunu inayoibua mafunzo aali
yanayowagusa watoto, wakongwe, vijana, wanaume, wanawake, wageni,
na wenyeji.
NATHAN WANGILA WANYONYI
DORINE CHAN.
Bi Doreen Chan (Kadika Girls)
Victoria Muasya
Edwin A Ombasa
Edwin A Ombasa
Edwin A Ombasa
WORNICKS GISEMBA
Enoch Osugo
Susan Munyi