Kitabu hiki kimeandikwa kwa uzingativu mkubwa unaolenga kuyakidhi mahitaji ya wanafunzi wote wa shule za upili na hata walimu. Kimezingatia silabasi ya Kiswahili kuanzia
kidato cha kwanza hadi kidato cha nne katika Matumizi ya Lugha
Kitabu hiki kinahusisha matini ambayo yamezikusanya mada zote na kuziwasilisha kwa
lugha nyepesi na sahili. Kinaweza kueleweka kwa urahisi na wanafunzi. Kimewasilisha
vipengele vyote kwa namna itakayorahisishia wanafunzi na vilevile walimu ujifunzaji na
ufundishaji. Vipengele hivi vimewasilishwa pamoja na mifano na hata mazoezi ya maswali
ya KCSE kutolewa kila baada ya mada na majibu yake kutolewa kulingana na miongozo yake
ya KCSE.
Mada za silabasi zimepanguliwa na kupangwa upya ili kuwasilishwa kwa mfululizo kuanzia
mada za kidato cha kwanza hadi kidato cha nne. Kitabu hiki hivyo basi kitamfaa sana mwanafunzi yeyote aliye na ari ya kujisomea na hata kupiga hatua mbele ya mwalimu. Kimewasilisha maswali ya KCSE kuanzia mwaka wa 2006 hadi sasa. Maswali hayo ya KCSE vilevile
yamepanguliwa na kupangwa upya kulingana na mada na majibu yake kutolewa nyuma ya
kitabu hiki. Mwanafunzi anayejitayarisha kwa mtihani wa KCSE atapata mwelekeo bora
kupitia kitabu hiki ili kumuwezesha kufaulu vyema katika Kiswahili.
Ningependa kuchukua nafasi hii kuwapendekezea walimu wakuu wa shule mbalimbali nchini, walimu wa Kiswahili na wanafunzi wapendao matokeo bora kujinyakulia nakala ya kitabu
hiki ili kiwanufaishe. Ahsanteni.
1. Zaidi ya wote, ni kumshukuru Mola, Rabuka kwa Neema zake za Uhai na Maarifa.
Samwel Ochiel Owino
Michael Latim Kegode
Bi Wamaitha (Utumishi Academy)
Bi Doreen Chan (Kadika Girls)
Michael Latim Kegode
Samwel Ochiel Owino
DORINE CHAN.
Bi Wamaitha (Utumishi Academy)
Peter M Kamau
Peter M Kamau
Samwel Ochiel Owino
Michael Latim Kegode
Michael Latim Kegode
VINCENT MUIRURI