MARUDIO KAMILIFU YA KISWAHILI: FASIHI SIMULIZI Kwa Shule za Upili
ByMichael Latim Kegode
Price
KES 10.0
Soft Copy Available
About this Book
Kitabu hiki cha Fasihi Simulizi kinahusisha matini ambayo
yamevikusanya vipera vyote vya fasihi simulizi na kuviwasilisha kwa
lugha nyepesi na sahili. Pia kimeshughulikia aina za mashairi na vigezo
mbalimbali vya kuyaainisha mashairi. Lengo la kufanya hivyo ni
kuwawezesha wanafunzi kujisomea na kufanya utafiti wa ziada wakiwa
na msingi bora katika sehemu hizi.
Kitabu hiki kitamfaa sana mwanafunzi yeyote aliye na ari ya
kujisomea na hata kupiga hatua mbele ya mwalimu. Kimewasilisha
maswali ya KCSE kuanzia mwaka wa 2006 hadi sasa. Mwanafunzi
anayejitayarisha kwa mtihani wa KCSE atapata mwelekeo bora kupitia
kitabu hiki ili kumwezesha kufaulu vyema katika Kiswahili.
Ningependa kuwahimiza wanafunzi kukipitia kitabu hiki kabla ya
kukumbana na mtihani wao. Kwa kufanya hivyo watakuwa na chukua
nafasi hii kuwapendekezea walimu wakuu wa shule mbalimbali
nchini, walimu wa Kiswahili na wanafunzi wapendao matokeo bora
kujinyakulia nakala ya kitabu hiki ili kiwanufaishe. Ahsanteni.