Kitabu hiki kimeandikwa kwa uzingativu mkubwa unaolenga kuyakidhi
mahitaji ya wanafunzi wote wa shule za upili na hata walimu. Kimezingatia silabasi ya Kiswahili kuanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha
nne katika Isimujamii
Kitabu hiki kinahusisha matini ambayo yamezikusanya mada zote na
kuziwasilisha kwa lugha nyepesi na sahili. Kinaweza kueleweka kwa
urahisi na wanafunzi. Kimewasilisha vipengele vyote kwa namna itakayorahisishia wanafunzi na vilevile walimu ujifunzaji na ufundishaji.
Vipengele hivi vimewasilishwa pamoja na mifano na hata mazoezi ya
maswali ya KCSE kutolewa kila baada ya mada na majibu yake kutolewa kulingana na miongozo yake ya KCSE.
Mada za silabasi zimepanguliwa na kupangwa upya ili kuwasilishwa
kwa mfululizo kuanzia mada za kidato cha kwanza hadi kidato cha nne.
Kitabu hiki hivyo basi kitamfaa sana mwanafunzi yeyote aliye na ari
ya kujisomea na hata kupiga hatua mbele ya mwalimu. Kimewasilisha
maswali ya KCSE kuanzia mwaka wa 2006 hadi sasa. Maswali hayo ya
KCSE vilevile yamepanguliwa na kupangwa upya kulingana na mada
na majibu yake kutolewa nyuma ya kitabu hiki. Mwanafunzi anayejitayarisha kwa mtihani wa KCSE atapata mwelekeo bora kupitia kitabu
hiki ili kumuwezesha kufaulu vyema katika Kiswahili.
Samwel Ochiel Owino
Michael Latim Kegode
Bi Wamaitha (Utumishi Academy)
Bi Doreen Chan (Kadika Girls)
Michael Latim Kegode
Samwel Ochiel Owino
DORINE CHAN.
Bi Wamaitha (Utumishi Academy)
Peter M Kamau
Peter M Kamau
Samwel Ochiel Owino
Michael Latim Kegode
Michael Latim Kegode
VINCENT MUIRURI